Roberto Mancini |
Kocha
wa klabu ya manchester city muitaliano Roberto
Mancini amekata tamaa na kusema kuwa timu yake kubaki katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya
itakuwa ni maajabu.
Kauli
hiyo imekuja Kufuatia klabu ya Manchester
city kupoteza mchezo wake dhidi ya klabu ya Ajax kwa kuambulia kipigo cha goli 3-1 katika
michuano ya ligi ya mabingwa barani
ulaya(UEFA)
Roberto Mancini, “Ni ngumu sana kwa sababu
kuna timu zenye pointi 7,nyingine pointi 6,pointi 3 hivyo itakuwa ni maajabu
kuendelea kwa hatua inayofuata”
Akizungumizia
hali ya mchezo Mancini amesema timu yake ilicheza vibaya kulinganisha wa
wenyeji wao timu ya Ajax.
“ Tumecheza
mpira wenye kiwango kibovu,tumepata nafasi chache lakini tumeshindwa
kufunga kutokana na kiwango kibovu cha walichoonesha wachezali”,alisema
kocha Roberto Mancini.
JOE- HART akiwa amelala baaada ya kumalizika kwa dk 90 huku wakiwa wamefungwa goli3-1 |
No comments:
Post a Comment