Zimebakia takribani siku 86 kwa wapenzi wa soka barani Afrika na duniani kuelekea Bondeni kwa mzee Mandela ambako michuano ya kuwania kombe la mataifa ya afrika (AFCON) itafanyika huku ile droo ya makundi imekwishafanyika na kushuudia mabingwa wa kombe hilo timu ya taifa ya Zambia ikiwa kundi moja na timu ngumu ya Nigeria,burkinafaso pamoja na Ethiopia.
Makundi ya timu zitakazoshiriki michuano hiyo ni
Group A: South Africa, Morocco, Cape Verde, Angola
Group B: Ghana, Mali, Niger, DR Congo
GROUP C: Zambia, Ethiopia, Burkina Faso, Nigeria
Group D: Ivory Coast, Togo , Algeria, Tunisia
Katika makundi haya kundi linalotazamiwa kuwa gumu ni kundi D pamoja na kundi B kwani makundi haya mawili yamebeba timu kongwe na ngumu.kwa mfano kundi D lenye timu za ivory cost ambao walikosa ubingwa huo mwaka huu kwa kufungwa na timu ya Zambia kwa njia ya peniti.
Timu ya taifa ya Afrika kusini |
Timu ambayo inayotazamiwa kuleta upinzani katika kundi hili ni timu ya taifa ya Tunisia,pamoja na hawa Algeria ambapo kwa kawaida timu hizi za mafia za kiarabu zimekuwa zikileta ugumu kwa timu hizi za asili za kiafarika.
Katika kundi B hili nalo ni kundi gumu zaidi kwani limekutanisha timu ngumu kama Mali,DR Congo ambapo timu kama ya Ghana inauchu mkubwa sana wa kutwaa taji hili.
timu ya taifa ya zambia |
Bingwa mtetezi yeye katika kundi lake si gumu sana pengine ukilinganisha na kundi A kwani Zambia hatapata upinzani mgumu kama atakaopata Ghana itakapocheza na Mali au congo ila ugumu utakuja pindi Zambia atakpocheza na timu ya taifa ya Nigeria
Hata Ethiopia,Burkinafaso, si timu za kubeza kwani nazo zimejianda vya kutosha katika kuelekea huko afrika kusini.
Didier Drogba. |
No comments:
Post a Comment