Herve Renard -Kocha wa zambia |
Timu za taifa za Zambia na Uganda zimekutana takribani mara kumi na tano katika michuano mbali mbali kama vile kufuzu kucheza kombe la dunia,michuano ya afrika mashariki na kati maarufu kama challenge cup ambapo timu ya taifa ya Uganda ndo inaongoza kwa kushinda mechi 8 kati ya 15 hali ya kuwa timu ya taifa ya Zambia imeshinda mechi 7
Ushindani wa timu hizi mbili ulianza mwaka 1973 katika michuano ya afrika mashariki na kati maarufu kama challenges cup ambapo Uganda walikuwa wenyeji wa michuano hiyo
vijana wa zambia wakipasha kuelekea mchezo dhidi yaa uganda |
Katika mashindano hayo timu hizo zilifanikiwa kutinga fainali ambapo mchezo wa kwanza zilitoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1 na ndipo mchezo wa marudiano ukapangwa kuchezwa siku inayofuata ambapo timu ya taifa ya Uganda ikafanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 kwa kutoka nyuma huku magoli hayo yakifungwa na Polly Ouma pamoja na Stanley “Tanker” Mubiru.
Mwaka 1974 timu hizi zilikutana tena katika michuano ya mataifa ya Afrika kwenye hatua ya makundi huku kundi hilo lilikuwa na wenyenji timu ya Taifa ya Misri,Ivory cost pamoja kundi hilo kuwa natimu ngumu timu ya taifa ya Zambia ilifanikiwa kusonga mbele kwa kuifunga timu ya Uganda goli moja kwa bila wakati wa mchezo wa mwisho wa kutafuta timu itakayoingia fainali.
Ushindani huo uliendelea kuzitawala timu hizi mbili za Uganda pamoja na timu ya taifa ya Zambia kuazia mwaka huo wa 1973 hadi 1992.
Bobby Williamson-kocha wa uganda |
Mwaka 1977 waweza sema ndio mwaka ambao unahisitoriya kubwa kati ya Tanzania na Uganda kwani mwaka huo dio vita baina ya tanzania na uganda ndio ilitokea
Mwaka huo mashindano ya michuano ya kombe la afrika mashsriki na kati maarufu kama challenges cup yalifanyika huko Somalia katika mji wa Mogadishu,nchini Somalia.timu hizi zilikutana kwenye mchezo wa fainali
Katika mchezo huo wa fainali Uganda walifanikiwa kuibuka na ushindi kwa kuifunga Zambia goli 5-3 kwa njia ya penaiti kwani timu hizo zilimalizika dk 120 zikiwa zimetosha nguvu nguvu huku shukrani za kipekee zimuende golikipa wa Uganda wakati ule waya Paul Ssali kwa kuibuka shujaa kwa kuokoa penaiti mbili za Zambia.
kikosi cha uganda kikiwa mazoezini |
Mchezo ambao timu ya taifa ya Uganda hauta usahau ni wa mwaka 1988 ambapo timu hiyo ilikubali kipigo cha jumla ya magoli 6-2 katika mchezo wa kuwania kushiriki michuano ya olimpiki yaliyofanyika huko korea.
Mechi ya kwanza ilichezwa Uganda ambapo wenyeji Uganda walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 huku magoli hayo yakifungwa na wachezaji kina Magid musisi pamoja na Ronald Vubya .
kikosi cha timu ya taifa cha uganda |
Inasemekana timu ya taifa ya uganda ilijichimbia kabri lake kwani kabla ya mechi ya marudiano mchezaji John Latigo ambaye alikuwa beki wakutegemewa upande wa kulia aliondolewa kwenye kikosi hicho na kocha Edward senkwangu kutokana na utovu wa nidhamu ambapo mchezaji huyo alitoloka wakati timu hiyo ikiwa kambini kwa ajiri ya kuwakabili wanachipolopolo.
Mchezo wa pili wa marudiano ulichezwa huko Zambia na timu hiyo ya Uganda ilipokea kipigo cha goli 5-1 kutoka kwa vijana hao wa Zambia akiwemo mchezaji Kalusha Bwalya
kikosi cha timu ya taifa-Zambia |
No comments:
Post a Comment