| AUGUSTIN SENGHOR -RAISI SHIRIKISHO LA MPIRA SENEGAL |
Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Senegal Augustin Senghor amesema yeye pamoja na kamati ya utendaji ya shirikisho hilo hawezi kujiuzuru kutokana na tukio la vurugu zilizotokea wakati wa mchezo kati ya timu ya taifa ya nchini senegal walipokuwa wameikaribisha timu ya taifa ya ivory cost kwa ajiri ya kuwania nafasi ya kuelekea afrika kusini kutakochezwa michuano ya kuwania kombe la mataifa afrika maarufu kama AFCON mwaka 2013 ambapo mchezo huo ulivunjika katika dk ya 76 hali ya kuwa wageni ivory wakiwa mbele kwa goli 2-0
baadhi ya mashabiki wa nchini senegal wakati wa vurugu. |
Augustin senghor, “Sisi tumechaguliwa kwa mkataba wa miaka minne,bado hatujafikia hata robo ya malengo yetu tulioazimia kuyatekeleza kabla ya mda wetu kumalizika,hivyo hatuwezi kujiuzuru kutokana na vurugu hizo za jumamosi na hao wanaotaka sisi tuondoke madarakani wanapoteza mda wao”.
Pia raisi huyo amesema vurugu hizo za jumamosi zimesabishwa na mtu mmoja hasiye na mapenzi ya dhati ya kuendeleza mpira nchini humo ambaye alitoa pesa kwa vijana wafanye fujo na ikumbukwe kuwa siku zilizopita shirikisho hilo lilimshutumu mchezaji El Hadji Diouf kuwa ndo chanzo cha vurugu hiyo
El Hadji Diouf |
No comments:
Post a Comment