Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo

Tuesday, November 6, 2012

Ramsey kuukosa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Schalke 04.


Aaron  Ramsey


Kiungo wa klabu ya Arsenal ya nchini uingereza  Aaron Ramsey  atakosa mchezo wa ligi ya mabingwa  barani ulaya  pindi klabu yake itakapocheza na klabu ya  Schalke 04 ya nchini ujerumani  jumanne ya  wiki kutokana na kuwa majuruhi.

Ikumbukwe katika mchezo wa ligi kuu  ya nchini humo jumamosi ya wiki iliyopita dhidi ya Manchester united na kuambulia kichapo cha  goli 2-1  kiungo huyo  Ramsey alitolewa katika kipindi cha pili  na nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji Johan Djourou.

Klabu ya Esparance yazikimbiza klabu za ulaya katika timu bora mianne za duniani,huku sudani ikiwakilishwa na klabu mbili katika takwamu hizo .



Klabu ya Barcelona


Shirikisho la kimataifa linalohusiana  na masuala ya takwimu na historia ya masuala ya mpira wa miguu duniani (IFFHS )limetangaza  takwimu ya  timu  bora  mianne za mwezi wa kumi huku  vinara wa ligi kuu ya nchini uhisipania Klabu ya Barcelona  ikiongoza kwa kushika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 349  ikifuatiwa na mabingwa wa ligi hiyo klabu yab real madridi wao wakiwa na pointi 290 huku klabu ya boca juniors ikishika nafasi  ya 3 kwa kuwa na  pointi 276

Licha  ya hivyo klabu nazo  za afrika zimefanikiwa kuingia katika timu mia moja bora  ambapo klabu hizo ni Klabu ya  Esperance   Tunis ya  nchini Tunisia ikishika nafasi ya  61 kidunia kwa kuwa na pointi  148.5  huku kwa afrika ikiwa nambari moja  na Al Hilal Omdurman ya nchini Sudani ikiwa na 129  huku ikishika nafasi ya  82

 

klabu ya Esparance

Klabu hiyo ya esparance imefanikiwa kuzibwaga klabu toka  barani ulaya kama klabu ya Fc Porto  yenyewe ikishika nafasi ya 71,Lille 77,Bordeaux79, na New castle 83

Klabu zilizofanikiwa kuongoza hapa afrika  ukiachana na hizo mbili zingine zilizotinga kumi bora afrika ni  Al-Merreikh Omdurman ya Sudan nafasi ya 3 ikiwa na pointi 113.5 ikifuatiwa na  Chelsea FC Berekum  ya nchini Ghana 4 ikiwa na pointi 113 , Wydad Casablanca ya  Morocco   nafasi ya  5 ikiwa na  poniti104.5 ,  timu nyingine ni Djoliba AS ya nchini mali, Al Ahly  ya nchini Egypt, 8- Sunshine Stars  ya nchini Nigeria, Desportivo Interclube ya nchini  Angola na inayofunga dirisha ni timu ya  Stade Malien ya nchini Mali ikiwa na pointi 81

Thursday, November 1, 2012

Gervinho nje kwa wiki 3.

GERVINHO



 Mshambuliaji  wa klabu ya arsenal  Gervinho  atakuwa  nje  ya uwanja  kwa takribani  wiki  3  kutokana  na kusumbuliwa  na tatizo  la kifundo  cha   mguu(aknkle)  ambapo alikumbwa na tatizo   hilo wakati  wa mchezo wa ligi  dhidi  ya QPR  wiki iliyopita.

 Hivyo  Gervunho ,Wojciech Szczesny, beki wa kushoto Kieran Gibbs pamoja  na kiongo Abou Diaby   wataikosa  mechi  dhidi ya  mashetani  wekendu  klabu  ya Manchester  united  huko Old  Trafford  jumamosi   ya wiki hii.


Uhondo wa wikii hii katika uwanja wa soka duniani.

KAGERA SUGAR.

Kwa kuanza  hapa  nyumbani kutakuwa na muendelezo  wa mechi  za ligi kuu Tanzania bara  ambapo  mchezo  unatazamiwa  kuwa  mgumu  ni  kati  ya  Klabu  yak ager sugar  wao watakuwa nyumbani kaitaba  kucheza na maafande  Tanzania  prison  kutoka  mbeya.


kIKOSI  CHA ESPARANCE

Mechi kali zitakazochezwa  wikendi   hii  barani  Afrika  kutakuwa  na fainali  ya kwanza ya ligi ya mabingwa  barani   afrika  ambapo klabu ya Al Ahly itakuwa  nyumbani kuikaribisha  klabu ya Esparance  ya nchini Tunisia

 

SAINT  CAZORLA

Uko barani ulaya  kubwa zaidi   ni mchezo kati  ya  klabu ya Manchester united   watakao  kuwa  nyumbani  Old  Trafford   kuwakaribisha  washika  bunduki wa jiji  la  London  klabu ya  Arsenal  huku kukiwa  na maswali   je,washika   bunduki  hao watarudisha   kipigo walichokipokea   msimu   wa mwaka  jana  cha goli 8-2

 

ROBIN   VAN  PERSIE.

Mchezo  huu unatazamiwa  kuwa mgumu  kwa pande.pamoja   na  hilo  mashabiki  wengi  wa soka  watakuwa  wana hamu  kubwa ya kumuona mshambuliaji mahili ambaye  ukipita  mtaani  hususani  kwa mashabiki wa Manchester upenda  kumuita  robini magoli  kutokan na umahili wake   wa kufumania  nyavu,swali  je  atamfunga  mlezi wake aliyemlea hadi  kufikia  hapo..? dakika 90  ndizo zitakazo toa majibu  ya  maswali yote.

LUIS  SUAREZ

Wikendii hii tena  mchezo unaotazamiwa  kuwa mgumu  ni kati  ya majogoo wa london  klabu ya Liverpool walioambulia  kipigo  cha  goli 3-1 katika mchezo wa kuwania kombe  la capital one  ambapo  Liverpool  watakuwa nyumbani Anfield kucheza  na klabu ya Newcstle