Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo
Wednesday, October 31, 2012
Tuesday, October 30, 2012
Micha richards nje kwa wiki sita au nane
Micha Richard |
Beki wa timu ya taifa ya England pamoja na mbaingwa ligi kuu nchini uingereza klabu ya Manchester city Micah Richards atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita au nane kutokana na kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia mara baada ya kuamia katika mchezo wa ligi dhidi ya klabu ya Swansea city jumamosi ya wiki iliyopita
Tangu kuanze kwa ligi kuu ya nchini uingereza Richards amefakiwa kucheza mechi nne za ligi hiyo hii ni kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya goti.hivyo klabu ya Manchester city imefiksha majeruhi 3 wanaocheza safu hiyo ya ulinzi,wachezaji hao ni Maicon pamoja na Pablo zabaleta.
Falcao: kwasasa sina mpango wa kuondoka Atletico madrid
Radamel-Falcao |
Mshambuliaji mahili
anayecheza katika klabu ya Atletico Madrid mkolombia Radamel Falcao amesema
hafikirii kuondoka katika
klabu hiyo mara
baada ya kuisadia klabu yake
kupanda hadi nafasi ya pili nyuma ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Barcelona
"Kwasasa
Sina mpango wa kuondoka na wala sijawahi kufikiria kutaka kuondoka", alisema Falcao ambaye anarekodi nzuri ya upachikaji wa magoli kwani tangu
kuanze kwa ligi ya nchini uhispania
falcao ameweza kufunga magoli 10 akiwa nyuma ya vinara wa
upachikaji magoli kin Lionel Messi
mwenye magoli 13,Christiano Ronaldo akiwa na magoli 11.
Pia ikumbukwe siku
kadhaa zilizopita kulikuwepo uvumi kuwa mchezaji huyo anataka kujiunga na mabingwa wa ligi hiyo klabu ya Real Madrid
ambayo inashika nafasi ya nne katika
msimamo wa ligi hiyo
kocha wa timu ya taifa ya zambia Herve Renard amesikitishwa na kitendo cha timu ya taifa ya kenya kumteuwa Henry Michel kama kocha wa timu ya
![]() |
kocha-Herve RenardKocha wa timu ya taifa ya Zambia mfaransa Herve Renard ameshangazwa na kitendo cha timu ya taifa ya Kenya Harambee stars kumteuwa mfaransa mwenzake Henry Michel kama kocha mkuu wa timu hiyoKocha huyo amesema Henry Michel si chaguo sahihi kwa timu ya taifa ya Kenya kwani ni vema kwa timu ya taifa ya kenya kupata kocha ambaye ataendana na wachezaji ikiwemo kuwapa hamasa ya kucheza mpira“Kenya ina kila kitu lakini nafikiria ya kwamba imekosea kuchagua kocha ambaye hana atauwezo wa kuisaidia timu kwani Henry Michel rekodi yake ni mbaya hivyo kenya inahitaji kocha ambaye anauwezo mkubwa wa kufundisha na sio Henry”,Alisema kocha Herve Renard.Herve Renard ni kocha mwenye mafanikio makubwa katika timu ya taifa ya Zambia kwani amefanikiwa kutwaa kombe la mataifa ya afrika maarufu kama (AFCON) mwaka huu wa 2012 akiifunga timu ya taifa ya ivory cost kwa mikwaju ya penaiti,pia kocha huyo amefanikiwa tena kuipeleka Zambia katika michuano hiyo itakayofanyika huko nchini Afrika kusini mapema mwakani |
Stewart kurejea kuinoa klabu ya Azam
![]() |
kocha Stewart-Hall |
Kocha wa zamani wa klabu ya Azam Stewart Hall ambaye alijiunga klabu ya Sofa paka ya nchini Kenya anatazamiwa kurudi kukinoa kikosi chake cha zamani cha Azam mara baada ya kushindwa kukubaliana na klabu ya Sofa paka
Stewart amesema anarudi nchini Tanzania katika klabu yake ya zamani kwani klabu ya azam imemuomba msamaha kwa yale yote yaliyotokea.
Hivyo stewart ataingia nchini Tanzania siku ya jumatano majira ya usiku kwa ajiri ya kuja kuitumikia klabu yake ya zamani ya azam ambayo tayari imekwisha kumfukuza mrith wa Stewart hall kocha Boris Bunjak kutokana na kiwango kibovu kinachooneshwa na klabu hiyo ikiwemo kupoteza michezo yake ya ligi kuu Tanzania bara.
Kocha Stewart akiwa katika klabu ya sofa paka amefanikiwa kushinda mchezo mmoja wa ligi,akipoteza michezo 2 na kutoa sare michezo 2.
Stewart Alipokuwa katika klabu ya azamu kabla ya kutupiwa virago kocha huyo alifanikiwa kuipatia klabu ya azamu kombe la mapinduzi, kushika nafasi ya pili katika michuano ya Urafiki,ligi kuu Tanzania bara pamoja na michuano ya kuwania kombe la kagame.
kwa hali hii...Tutamaliza makocha wote bila hata mafanikio
kikosi cha Azam |
Klabu ya Azama maarufu kama wanaramba ramba imetangaza rasimi kumfukuza kocha wake Boris Bunjak kufutia matokeo mabaya katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara
Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu hiyo Patrick Kahemela amesema ni kweli kocha huyo amerushiwa virago kutokana na kuwa na matokeo mabaya ikiwemo hata kiwango kibovu kinachooneshwa na klabu hiyo kitu ambacho kinapelekea kupoteza kwa michezo yake na hivyo kujikuta klabu hiyo ikishuka hadi nafasi ya nne kutoka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara
Boris-Bunjak |
Kocka huyo anatazamiwa kuondoka nchini Tanzania kulekea nchini kwao siku ya alhamisi ya wiki hii huku kunatetesi kuwa kocha aliyetimuliwa Stewart Hall ndiy atakayekuja kukinoa kikoso hicho
Rekodi ya Bunjak tangu ajiunge na klabu ya azam amefanikiwa kushinda mechi nne, kutoa sare mara 3,na kupoteza michezo 2 huku mchezo wa simba ndio uliopelekea kocha huyo kufungishiwa virago mara baada ya kupokea kipigo cha goli 3-1
Hizi ni mechi ilizocheza klabu ya Azam ikiwa chini ya kocha Bunjak kabla ya kutimuliwa.
Azam 1-0 Kagera Sugar
Azam 2-2 Toto African
Azam 3-0 JKT Ruvu
Azam 1-0 Mtibwa Sugar
Azam 1-0 African Lyon
Azam 1-0 Polisi Morogoro
Azam 0-0 Prisons
Azam 1-1 Ruvu Shooting
Azam 1-3 Simba
Subscribe to:
Posts (Atom)

