Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (KRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika
jana (Oktoba 7 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa ARFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo
mkoani Kigoma.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya ARFA chini ya
uenyekiti wa Khalifa Mgonja ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli
za mpira wa miguu mkoani Arusha kwa kuzingatia katiba ya ARFA pamoja na vyombo
vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya ARFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa
kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Khalifa Mgonja (Mwenyekiti), Seif Banka
(Makamu Mwenyekiti), Adam Brown (Katibu), Peter Temu (Mjumbe wa Mkutano Mkuu
TFF), Omari Walii (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Mwalizo Nassoro (Mhazini).
Waliochaguliwa
kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika Leganga, Usa
River ni Hamisi Issa, Athuman Mhando na Eliwanga Mjema. Nafasi ya Katibu
Msaidizi iko wazi na itajazwa katika uchaguzi mdogo utakayofanyika baadaye.
No comments:
Post a Comment