Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo

Tuesday, October 30, 2012



ENDAPO HII TIMU IKIUNDWA KUWA TIMU MOJA ITAKUWA BONGE LA TIMU.

Wachezaji bora   wa mwezi wa kumi wanaounda kikosi cha kwanza   cha wachezaji  kumi na moja ambao wameonyesha kiwango cha juu kwa kuzisaidia timu zao  kupata ushindi katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara  mwezi huu wa kumi ni  wachezaji hao ni
1.Golikipa
Yaw   berko
2.Mabeki
Shomari kapombe, mbuyu twite,stephano mwasika,saidi choro,
3.Viungo
Mwinyi kazimoto,Haruna niyonzima,amri kiemba,
4.Washambuliaji
Edward  Christopher,Emanul Okwi,

Ukianza kuangalia kiwango cha mchezaji mmoja mmoja kati ya hawa bila shaka hutokuwa na wasiwasi hata kidogo kwani wachezaji hawa wameonyesha kiwango cha hali ya juu  katika michezo mbalimabli ya ligi kuu Tanzania bara  tangu kuanze kwa mwezi huu wa kumi,

Christopher Edward


Mchezaji kama Edward Christopher  ni mchezaji mwenye umri mdogo ukilinganisha na wachezaji kama vile kina tegete,Emanuel okwi,said bahanuzi ambaye amejipatia jina katika michuano ya kagame iliyofanyika mwaka huu hapa nchini Tanzania.

Pamoja na kuwa na umri mdogo kocha milovan cirkovic ameamua kumpa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hii ni kwasababu anajua kuwa Christopher anauwezo mkubwa wa kumiliki mpira,kufunga,kwa mfano wakati wa  mchezo wa maasimu wa jadi Simba na   Yanga kila mmoja hakutegemea kama christoper angestahimili kasi ya wakubwa zake,kuipa wakati mgumu ngome ya Yanga.
 
Hivyo   Christpher Edward ni mmja ya washambuliaji wazuri hapa Tanzania na akitulia,akafanya kazi kwa bidiii huku akiwa na malengo akilini mwake basi na yeye atafanikiwa kufuata nyao  za matanzania mwenzake Mbwana Samatha.
Kwa upande wa viungo sio siri wachezaji hawa wanafanya kazi.kiasi kwamba unapokuwa uwanjani alafu timu moja wapo ya wachezaji hawa iko nyuma kwa goli kadhaa utaona ni jinsi gani wanavyokuwa wanahaha kwa kutafuta mpira,kutengeneza mazingira ya kufunga na hata kutafuta nafasi ya wao kufunga   wao wenyewe.

Mwinyi kazimoto ambaye waweza sema ndio tegemeo kubwa kwa timu ya simba kiasi kwamba akiumia mashabiki na hata baadhi ya viongozi hupatwa  na wasiwasi mkubwa  wa nani atayeziba pengo hilo

Haruna   Niyonzima(Fabrigas wa afrika mashariki) hapa kwa wanayanga huwaelezi kitu chochote kuhusu kiwango cha Haruna ambaye si dhani timu ya yanga inaweza kumuuza kiurahisi amekuwa na mchano mkubwa sana katika safu ya kati ya timu ya Yanga.

Mbuyu Twite

Katika safu ya ulinzi hapo haina shida kwa kunavijana ambao wanajua wanachokifanya.mchezaji kama mbuyu twite ambaye alileta utata katika usjiri wa kuichezea timu Yanga naye pia  ameonesha kiwango cha juu.kwa  mfano katika mechi ya maasimu wa jadi simba na yanga sio siri Twite alionesha kiwango cha  juu zaidi,

shomari kapombe   ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa  wa kucheza  nafasi zaidi ya moja uwanjani. Kwa mfano katika mchezo wa ligi kati ya Timu ya Simba na Maasimu wa wakubwa Timu ya  Yanga  mwanzo mwa mwezi huu  shomari alionesha uhodaro mkubwa wa kuwahimli  washambuliaji wa Yanga kama  vile  Saidi Bahanuzi ambaye  ni moja ya wachezaji wasumbufu ,wenye nguvu  ambao uhitajika umakini  katika kuwakaba lakini siku hiyo  shomari kapombe alifanya kazi ya ziada.

Kwa upende wa golini hapo haina shida kwani mghana  berko ni moja ya golikipa wazuri katika ligi kuu   Tanzania  bara  licha  ya kuwa anasumbuliwa na majeruhi lakini bado anaonesha  umahiri wake




No comments:

Post a Comment