Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo

Tuesday, October 30, 2012

kwa hali hii...Tutamaliza makocha wote bila hata mafanikio

kikosi cha  Azam

Klabu ya  Azama  maarufu  kama  wanaramba ramba  imetangaza rasimi kumfukuza  kocha wake Boris  Bunjak kufutia  matokeo mabaya  katika  michuano ya ligi kuu Tanzania bara

Kwa mujibu wa Afisa  habari wa klabu hiyo  Patrick  Kahemela  amesema ni kweli kocha huyo amerushiwa virago kutokana na kuwa na matokeo  mabaya ikiwemo hata kiwango kibovu kinachooneshwa  na  klabu hiyo kitu ambacho kinapelekea kupoteza kwa michezo yake na hivyo kujikuta klabu hiyo ikishuka hadi nafasi ya nne kutoka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara

 

Boris-Bunjak

Kocka huyo anatazamiwa  kuondoka nchini  Tanzania  kulekea  nchini kwao siku ya alhamisi ya wiki hii huku kunatetesi kuwa  kocha aliyetimuliwa  Stewart  Hall ndiy atakayekuja kukinoa kikoso hicho

Rekodi ya  Bunjak  tangu ajiunge  na klabu ya azam  amefanikiwa kushinda  mechi nne, kutoa sare mara 3,na kupoteza  michezo 2 huku mchezo wa simba ndio uliopelekea kocha huyo kufungishiwa  virago  mara baada ya kupokea kipigo cha goli 3-1

 

Hizi  ni mechi ilizocheza klabu ya Azam  ikiwa chini ya kocha Bunjak kabla ya kutimuliwa.

Azam 1-0 Kagera Sugar

Azam 2-2 Toto African

Azam 3-0 JKT Ruvu

Azam 1-0 Mtibwa Sugar

Azam 1-0 African Lyon

Azam 1-0 Polisi Morogoro

Azam 0-0 Prisons

Azam 1-1 Ruvu Shooting

Azam 1-3 Simba

 

No comments:

Post a Comment