Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo

Friday, October 12, 2012

Chama cha soka cha Uruguay kimesema hakina imani na makamu rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, Jim Boyce


Luis Suarez  


Chama cha soka  cha  nchini  Uruguay  kimetangaza kutokuwa na imani na  Jim Boyce ambaye ni  makamu wa rais  wa shirikisho la  mpira  wa  miguu  duniani FIFA  na kuiomba bodi ichunguze  tabia  ya   Jim Boyce 

Hatua  hii imekuja  kufutia siku chache  zilizopita  makamu huyo kumshutumu  mchezaji wa Taifa hilo Luis   Suarez   kwa kitendo  chake cha kujiangusha  ndani ya  eneo la penaiti ili apewe peanaiti  ambapo  suarez alifanya  hivyo wakati  wa mchezo  wa ligi  kuu  nchini uingereza  dhidi ya  timu ya stoke  city.

Jim Boyce-Makamu rais Fifa


Barua  iliyotumwa  na chama chama cha soka  cha Uruguay  katika shrikisho la mpira wa miguu duniani  FiFA  inalalamikia  kitendo cha  makamu huyo  kutaka kuendeleza  chuki na uhasama miongoni mwa wachezaji 

Pia  barua hiyo inaeleza kwamba  kwa mujibu wa sheria na kanuni za  shrikisho  la mpira wa miguu duniani FIFA  linamtaka kila kiongozi ndani ya shikisho hilo kuheshimu taratibu zilizopangwa 

Hivyo kutokana  na makamu huyo kukiuka  moja ya sheria  hizo  Chama  hicho cha soka cha  ya Uruguay kimetangaza  kuwa  hakitatambua nafasi yake kama kiongozi ikiwemo  kutokuwa na imani naye kwani anachochea chuki  miongoni mwa wachezaji.

No comments:

Post a Comment