Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo

Wednesday, October 17, 2012

Ni bora tukacheze ligi ya visiwani,au mchezo wa bao kuliko kuvaa jezi yenye doa jekundu.Tamko la wazee wa timu ya Yanga.




Timu Yanga

Klabu ya soka ya mpira wa miguu nchini Tanzania,klabu ya yanga maarufu kama vijana wa jangwani leo hii kupitia kamati ya  wazee hiliyokaa tarehe 6.10.2012   kujadiri hatima ya klabu hiyo kuhusu kuvaa nembo yenye rangi nyekundu  hatimaye  wazee hao wametoa tamko kuhusiana na suala hilo na kusema wako tayari kucheza ligi ya Tanzania visiwani,au michezo mingine kama mchezo wa bao kuliko kuvaa jezi yenye nembo nyekundu.

 

Ibrahim-Akilimali-katibu wazee Yanga

    Akiongea na waandishi wa habari leo hii jijin dare s salaam katibu wa wazee wa klabu hiyo Ibrahim  Akilimali amesema  wanaishangaa kampuni ya simu ya Vodacom kwa kubadilika badilika kwani  mwaka jana Vodacom ilikubali ombi la klabu hiyo na kuweka nembo nyekundu,mwaka imkuwaje kwa kampuni hiyo kugeuka..?

    Ilikuhakisha kamati hiyo ya wazee ya klabu hiyo imeamua  kuwakubusha wanachama,kampuni ya simu ya Vodacom kuwa  mnamo mwaka 1955.22.08  wakati huo mdhamini wa klabu  hiyo alikuwa ndugu Abdallah Keremji,nchini ya uongozi wa Mzee  kondo s. kipwata

Kumbukumbu ni kwamba mwaka huo kuliandaliwa mechi kati ya klabu ya Yanga dhidi ya timu ya mabaharia ,mgeni rasimi wa mchezo huo alikuwa  Gavana Edward  Twining.

 Timu hiyo ya mabaharia ilikuja na jezi zao nyekundu  ili kuwapa yanga wazivae mbele  ya Mgeni rasimi lakini timu ya Yanga ilikataa na kusema wako tayari kucheza kifua wazi kuliko kuvaa jezi nyekundu

Vijana wa Yanga-Tegete,Niyonzima  na Chuji

  Pia katibu huyo ametoa mfano mwingine kwa kusema kuwa  mwaka huo huo wa 1995 chama cha TANU  kilitoa  rai kwa klabu hiyo kubadili rangi zake kwani chama hicho kinatumia rangi kama za timu ya Yanga,lakini Raisi wa kwanza wa Tanzania wakati huo  Mwl Nyerere akiwa mwenyekiti  wa chama cha TANU alikataa wazo hilo na kusema kuwa si sahihi kwani timu hiyo ni ya kwanza kutumia rangi hiyo.

 Hivyo akitoa tamko hilo kwa niaba ya kamati ya wazee wa klabu hiyo,katibu huyo wa wazee amesema   haitawezekana kuvaa  jezi yenye doa  jekundu  mpaka dunia itakapokwisha.

 

No comments:

Post a Comment