Radamel-Falcao |
Mshambuliaji mahili
anayecheza katika klabu ya Atletico Madrid mkolombia Radamel Falcao amesema
hafikirii kuondoka katika
klabu hiyo mara
baada ya kuisadia klabu yake
kupanda hadi nafasi ya pili nyuma ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Barcelona
"Kwasasa
Sina mpango wa kuondoka na wala sijawahi kufikiria kutaka kuondoka", alisema Falcao ambaye anarekodi nzuri ya upachikaji wa magoli kwani tangu
kuanze kwa ligi ya nchini uhispania
falcao ameweza kufunga magoli 10 akiwa nyuma ya vinara wa
upachikaji magoli kin Lionel Messi
mwenye magoli 13,Christiano Ronaldo akiwa na magoli 11.
Pia ikumbukwe siku
kadhaa zilizopita kulikuwepo uvumi kuwa mchezaji huyo anataka kujiunga na mabingwa wa ligi hiyo klabu ya Real Madrid
ambayo inashika nafasi ya nne katika
msimamo wa ligi hiyo
No comments:
Post a Comment