Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo

Thursday, November 1, 2012

Uhondo wa wikii hii katika uwanja wa soka duniani.

KAGERA SUGAR.

Kwa kuanza  hapa  nyumbani kutakuwa na muendelezo  wa mechi  za ligi kuu Tanzania bara  ambapo  mchezo  unatazamiwa  kuwa  mgumu  ni  kati  ya  Klabu  yak ager sugar  wao watakuwa nyumbani kaitaba  kucheza na maafande  Tanzania  prison  kutoka  mbeya.


kIKOSI  CHA ESPARANCE

Mechi kali zitakazochezwa  wikendi   hii  barani  Afrika  kutakuwa  na fainali  ya kwanza ya ligi ya mabingwa  barani   afrika  ambapo klabu ya Al Ahly itakuwa  nyumbani kuikaribisha  klabu ya Esparance  ya nchini Tunisia

 

SAINT  CAZORLA

Uko barani ulaya  kubwa zaidi   ni mchezo kati  ya  klabu ya Manchester united   watakao  kuwa  nyumbani  Old  Trafford   kuwakaribisha  washika  bunduki wa jiji  la  London  klabu ya  Arsenal  huku kukiwa  na maswali   je,washika   bunduki  hao watarudisha   kipigo walichokipokea   msimu   wa mwaka  jana  cha goli 8-2

 

ROBIN   VAN  PERSIE.

Mchezo  huu unatazamiwa  kuwa mgumu  kwa pande.pamoja   na  hilo  mashabiki  wengi  wa soka  watakuwa  wana hamu  kubwa ya kumuona mshambuliaji mahili ambaye  ukipita  mtaani  hususani  kwa mashabiki wa Manchester upenda  kumuita  robini magoli  kutokan na umahili wake   wa kufumania  nyavu,swali  je  atamfunga  mlezi wake aliyemlea hadi  kufikia  hapo..? dakika 90  ndizo zitakazo toa majibu  ya  maswali yote.

LUIS  SUAREZ

Wikendii hii tena  mchezo unaotazamiwa  kuwa mgumu  ni kati  ya majogoo wa london  klabu ya Liverpool walioambulia  kipigo  cha  goli 3-1 katika mchezo wa kuwania kombe  la capital one  ambapo  Liverpool  watakuwa nyumbani Anfield kucheza  na klabu ya Newcstle

No comments:

Post a Comment