Karibu katika dira ya michezo kwa habari motomoto za michezo ya ndani na nje ya nchi
Karibu katika dira ya michezo

Thursday, October 4, 2012

Tasimini ya mchezo wa watani wa jadi Simba VS Yanga.



Simba sport club.


 Bila shaka kama umefatilia mpra  wa jana wa maasimu wakubwa nchini Tanzania klabu za simba na Yanga  hautakuwa na walakini  kwa kiwango kilichooneshwa na timu zote  mbili.

Tukianza kuwazungumzia  wachezaji kama Edward Christopher ni kijana mdogo lakini jana ameonesha  uwezo wake na kuziba midomo ya baadhi ya watu waliokuwa wakisema hataweza kuhimili mikikiki ya wazee wa klabu za simba na Yanga.

Shomari kapombe akimzibiti Niyonzima

 

Kwa kifupi klabu ya simba ilikuwa imejipanga  vizuri kipindi cha kwanza ukitazama safu ya beki  unaona kabisa Shomari kapombe alivyokuwa anafanyakazi ya kumzibiti mashambuliaji  Saidi Bahanuzi. Pia katika safu ya  kiungo simba walikuwa wametulia wakikaba  kwa makini kitu ambacho kiliwapa shida Yanga waliokuwa wakiongozwa na mrwanda  Haruna niyonzima .

Kwa upande wa mbele palikuwa safi ila tatizo lilikuwa katika kumiliki mpira,kutoa pasi na hata kuunganisha krosi zilizokuwa zinzpigwa mara nyingi kutokea kwa Mrisho Ngasa.

Kikosi cha Da young Afrikani.

Hayo ni Simba kwa upande wa Yanga unaweza kusema kipindi cha  kwanza walikuwa wamelala kwani  hawakucheza kwa kiwango kilichokuwa kinategemewa na mashabiki wake  kutokana na usajiri wa klabu hiyo mshambuliaji aliyeng’ara katika michuano ya  kagame Saidi Bahanuzi kushindwa kuonesha cheche zake kwa kuzibitiwa na kinda  Shomari Kapombe aliyekuwa katika kiwango cha juu.

Mchezaji kama vile  Frank domayo aliyeingia kuchukua nafasi ya mganda Hamis kiiza kulionekana kuipa uhai yanga katika safu ya kiungo kitu ambacho kilibadilisha mchezo  kwa klabu ya Yanga kuanza kushambulia  kutokana kupata mtu wa kuwalisha washambuliaji kama vile Saidi Bahanuzi alieyeonekana kuisumbua ngome ya  simba.

Kwa upende wa refa wa mchezo huo kipindi cha pili alionekana kuyimba kimaamuzi  pengine ni kutokana na presha ya washibiki waliokuwa wakipiga kelele kuwa aidha atoe kadi au hasitoe.kwa mfano   mchezaji Haruna moshi Bobani alivyomchezea vibaya beki wa zamani wa simba Kelvin yondani.Waweza kusema hivi kama tukiacha maneno,fitina  na tukielekeza  jitihada zetu katika mpira kama walivyowenzetu tutafika mbali.

 

No comments:

Post a Comment