Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Oktoba 5
mwaka huu) kupitia na kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali na kupanga Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) ianze kutimua vumbi Oktoba 20 mwaka huu.
| Afisa habari-Boniface Wambura |
Afisa
habari wa TFF Boniface Wambura amesema timu
zimepangwa katika makundi matatu ya timu nane nane ambapo zitacheza ligi hiyo
kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Mshindi wa kila kundi ndiye atakayepata
tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao wakati timu ya mwisho
kila kundi itashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa.
Wambura
ameyataja makundi ambapo Kundi A lina timu za Burkina Moro ya Morogoro,
Kurugenzi Mufindi ya Iringa, Majimaji ya Songea, Mbeya City ya Mbeya, Mlale JKT
ya Ruvuma, Mkamba Rangers ya Morogoro, Polisi Iringa na Small Kids ya Rukwa.
Ndanda
FC ya Mtwara, Ashanti United, Green Warriors, Moro United, Polisi, Tessema,
Transit Camp na Villa Squad zote za Dar es Salaam ndizo zinazounda kundi B
wakati kundi C ni Kanembwa JKT ya Kigoma, Morani ya Manyara, Mwadui ya
Shinyanga, Pamba ya Mwanza Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino
Rangers ya Tabora.
No comments:
Post a Comment