UONGOZI WA YANGA WAMTIMUA KOCHA
WAKE
Uongozi wa klabu ya sokaya Yanga umesitisha mkataba wa
kocha wake mkuu Tom Saintfiet pamoja kuwaengua katibu mkuu ,meneja pamoja na
msemaji wa klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya mitaa ya twiga na jangwani
![]() |
aliyekuwa kocha wa Da Young African -Tom Saintfiet |
Ilikuwa hali ya shamra shamra kwa wanachama na mashabiki
wa klabu ya Yanga wakati wakati
wakimpokea kocha Tom Saint fiet kuja kuchukua nafasi ya Kostadin Papic
aliyetimuliwa kikosi hapo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kumalizika kwa
ligi kuu msimu uliopita
Maisha ya kocha Tom Saitfiet klabuni hapo yamedumu kwa miezi miwili tu baada ya uongozi wa klabu hiyo kusitisha mkataba na kocha huyo raia wa ubelgiji kutokana
na kushindwa kuendana na mipango ya klabu hiyo
Makamu mwenyekiti
wa wanajangwani Clement Sanga amedai kuwa uongozi umefikia hatua ya
kusitisha mkataba na kocha huyo kwa kuwa
ameshindwa kusimamia mipango ya klabu
ambapo alikataa timu kuiweka kambini muda mrefu na badala yake kutaka ikae siku tatu kabla ya
mechi
Uongozi huo umempa majukumu ya ukocha mkuu Fred Felix
Minziro kwa sasa mpaka atakapopatikana kocha mwingine atakayekinoa kikosi hicho
![]() |
aliyekuwa katibu wa YANGA-Celestine Mwesigwa |
Katikamabadiliko hayo pia uongozi umemtangaza mchezaji
wa zamani wa klabu hiyo Lawrence Mwalusako kukaimu nafasi ya katibu mkuu baada
ya kusimamishwa kwa aliyekuwa katibu wa
timu hiyo Celestine Mwesigwa huku Denis
Oundo akiteuliwa kuwa mkurugenzi wa fedha na utawala
![]() |
Wana wa Jangwani YANGA |
Tom Saintfiet amedumu katika kikosi cha Yanga kwa muda
wa miezi miwili tu baada ya kutimuliwa kwa kocha Kostadin Papic aliyechukua mikoba ya mganda Sam Timbe ambaye naye alitimuliwa kikosini hapo baada ya kukaa na kikosi hicho na kutwaa
ubingwa wa ligi kuu



No comments:
Post a Comment